Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema jumla ya Wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na ugonjwa wa  #COVID19 huku Wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, wagonjwa 7 wako kwenye uangalizi maalum (ICU), 11 wamepona na 10 wamefariki

Mara ya mwisho Waziri wa Afya alitoa taarifa kuwa jumla ya visa vya wagonjwa wa COVID19 ilikuwa 254 baada ya Wagonjwa 84 kuongezeka

Aidha, Waziri Mkuu amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na Wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 waliokutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284)

Waziri Mkuu ameyasema hayo akiwa kwenye Maombezi ya kuombea Taifa dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona yanayofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar

Pia, amsema Rais Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu wamemtuma awasilishe salamu za upendo na shukrani kwa wote wanaoonesha jitihada katika kupigania maisha ya watu wote hapa nchini.

 

Mpaka sasa watu 2,571,660 wameambukiwa virusi hivi duniani kote huku vifo 178,281 vikirekodiwa duniani 

Share with Others