Maduki, ambaye alishtakiwa kwa makosa 280 yakiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo pamoja na utakatishaji fedha, ameteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta).


Mashtaka yao yalisomwa Januari 6 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, lakini ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma (DPP) ililiondoa shauri hilo siku iliyofuata baada ya kuonyesha nia ya kutoendelea na kesi hiyo.


Siku hiyo, Maduki na mhasibu wa Wizara ya Afya, Luis Lymo (54) ambaye hakuwapo mahakamani, walisomewa mashtaka na mawakili wa Serikali, Zakaria Ndaskoi na Genes Tesha mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Augustina Mmbando.


Wakati kesi hiyo iliyokuwa imeahirishwa ikisubiri kutajwa, Maduki, ambaye ni mtendaji mkuu wa taasisi ya Christian Social Services Commission, juzi aliteuliwa na Rais Magufuli kuendelea kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo ya Veta.


Baada ya taarifa ya uteuzi huo waandishi wa habari waliambiwa ofisi ya DPP haikuonesha nia ya kuendelea na kesi hiyo huku wakili wa Serikali, Genes Tesha akieleza kuwa kesi hiyo iliondolewa mahakamani siku moja baada ya kufunguliwa.

Share with Others