Katika kuelekea sikuu ya Christmas, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Christine Kayendeke, amenusurika kifo kwa kushambuliwa na mume wake Peter Kadama (50), baada ya kumchinja jogoo aliyepangwa aliwe siku ya sikukuu ya krismass.

Imeelezwa kuwa mwanaume huyo mkazi wa nchini Uganda,  alimnunua kuku huyo kwa pesa ya Uganda Shilingi 15,000/=,  kisha kumpeleka kwa Mke na kutoa maagizo kwamba atachinjwa katika sikukuu hiyo.

Mkewe alikiuka maagizo na kumchinja siku ya Jumapili ya Disemba 15,2019, ndipo Mume wake alipatwa na hasira kisha kumpiga nusura ya kumuua.

Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa eneo hilo Joseph Gadimba amesema kuwa, “Mwanaume alimpiga sana Mke wake nusura ya kutaka kumuua, Mwanamke huyo kwa sasa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Budaka, kesi hii bado haijafika Polisi ila tumeamuru mwanaume huyo anatakiwa atimize majukumu ya kumgharamia hadi atakapopona”.

Aidha Gadimba ameongeza kuwa “Mwanamke atakapopata nafuu ndugu na wazazi  wa pande zote mbili watafanya kikao ili kumaliza tofauti zao nakuwaunganisha tena wakae pamoja”.

Share with Others