Mkazi wa Rutamba mkoani Lindi Hemedi Ali Hassan (33) amekutwa ameuawa na watu wasiofahamika kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali  huku wauaji hao wakichukua pikipiki yake aina ya SANLG.

Tukio hilo limetokea Novemba 17 2019 majira ya saa Sita mchana ,ambapo mwili wake uligundulika katika maeneo ya Makongole Rutamba manispaa ya LIndi ukiwa unamajeraha sehemu za shingoni ,mgongoni, kifuani na ubavuni.


Shuhuda katika tukio hilo  ambaye pia ni ndugu wa karibu wa familia ya marehemu ,HAMAD MTOPA amesema baada ya kupata taarifa za kutorudi nyumbani kwa HEMED kutoka kwa mke wake walianza kumtafuta na kuukuta mwili na Helment ya pikipiki kwenye  mkorosho.Kamanda wa polisi Mkoani Lindi PRUDENSIANA PROTAS amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi bado linaendelea kufanya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
 

Share with Others