Ripoti ya pamoja iliyochapishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kiliomo (FAO) na mashirika mengine manne ya umoja huo yanayohusika na suala hilo inaonyesha kwamba njaa ulimwenguni iliongezeka mnamo mwaka 2017, kwa mwaka wa tatu mfululizo.
José Graziano da Silva, Mkurugenzi Mkuu wa FAO ameelezea masikitiko yake, akisema "kwa bahati mbaya habari kubwa siyo habari njema ... Kwa mwaka wa tatu, napaswa nitangazie kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani imeongezeka. "
Karibu watu milioni 821 walikabiliwa na njaa ulimwenguni mnamo mwaka 2017, ikilinganishwa na 804 mnamo mwaka 2016. Afrika bado inaendelea kuathirika zaidi ikiwa na asilimia 21 ya watu wanaokula vibaya, ikifutiwa na Asia ambayo  inachukuwa nafasi ya pili kwa 11.5 %.
Idadi watu wanaokabiliwa na njaa imerejea kwenye kiwango chake cha miaka kumi iliyopita. Ambapo kwa mujibu wa FAO inasema hali hiyo imesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa: "Mwaka huu suala la mabadiliko ya hali ya hewa litazingatiwa zaidi. Ripoti hiyo inaonyesha wazi kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, na kutokea kwa majanga mbalimbali ya asili, vimeweka hatarini maendeleo na taratibu za kuondokana na njaa na utapiamlo, "ameongeza José Graziano da Silva.
Pia Mashirika hayo yamebaini kwamba watoto milioni 151 wanakabiliwa na njaa.
Miaka kumi na nane iliyopita, Umoja wa Mataifa ulijitoa kuhakikisha hadi mwaka  2030 kuondokana na njaa duniani. Lengo hili nzuri linaonekana limekosa mwelekeo.
 

Share with Others