Bei ya korosho kwa mnada wa tano, msimu wa 2019/2020 katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, mkoa wa Lindi imeongezeka ikilinganishwa na mnada wa wanne.

 

Meneja mkuu wa chama cha umoja Liwale Jahida Hassan amesema bei ya juu katika mnada huo ni shilingi 2,857 kwa kila kilo moja. huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,817.

 

Jahidi amesema bei hizo ni tofauti na bei za mnada wa nne uliofanyika wilayani Nachingwea katika viwanja vya ofisi za chama kikuu hicho ambapo bei ya juu ilikuwa shilingi 2,812 na bei ya chini ilikuwa shilingi 2,795 kwa kila kilo moja.

 

Jahidi ameongeza kuwa katika ghala la Umoja lililopo Liwale kampuni ya Royal nut ilinunua tani 158 kwa bei ya shilingi 2,857 kwa kila kilo moja, kampuni ya Kasuga tani 150 kwa bei ya shilingi 2,857, 

 

Mbali na maghala hayo makuu mawili yaliyopo katika wilaya za Nachingwea na Liwale. Meneja huyo amezitaja kampuni zilizonunua korosho zilizopo katika ghala la Lipande wilaya ya Ruangwa.

 

Alisema katika ghala hilo la Lipande kampuni ya Iscon imenunua tani 459 kwa bei ya shilingi 2,826, kampuni ya MGM tani 250 kwa bei ya shilingi 2,819. Wakati kampuni ya Iscon kwa mara nyingine kwenye ghala hilo imenunua tani 144 kwa bei ya shilingi 2,817.

Share with Others