Benki ya Dunia yazuia msaada wa zaidi ya tsh. bilioni 112 kwa Tanzania ikipinga sheria ya Takwimu ikisema ni kutokana na kukandamizwa kwa uhuru wa maoni hususani kuhusu Takwimu za Tanzania

Kwa mujibu wa taarifa ya Benki hiyo kama ilivyotolewa katika mtandano wa Eyeonglobaltransparency.net inasema ni kutokana na kukandamizwa kwa uhuru wa maoni hususani kuhusu takwimu za Tanzania

Benki hiyo imewasilisha wasiwasi wake kwa Serikali ya Tanzania na kwamba bado wanafanya mazungumzo na Mamlaka husika juu ya Sheria hiyo ya mwaka 2015 iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni

Inasema sheria hiyo "haifungamani na viwango vya Kimataifa kama vile Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa za Takwimu Rasmi na Mkataba wa Afrika wa Takwimu."

Sheria hiyo inakataza usambazaji wa takwimu zozote zinazopotosha au kupingana na takwimu rasmi zinazotolewa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa huku atakayekiuka atalipa faini ya zaidi ya Tsh. Milioni 13 au kifungo cha miaka mitatu
 

Share with Others