Bibi wa Kambo wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama amefariki Dunia katika hospitali nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99.


Mama Sarah amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu na amefariki alipokuwa akipatiwa matibabu  katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga Iliyopo Kisumu nchini humo huku familia yake ikiwa inafanya mipango ya kufanya mazishi yake Leo Machi 29,2021 katika makaburi ya Umma


Mpaka sasa tayari Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameelezea masikitiko yake na kutuma salamu za rambirambi kwa Familia ya Obama kufuatia kifo cha ni Bibi huyo wa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama  na kusema hili ni pigo kwa Taifa letu, tumempoteza Mwanamke shupavu, aliyeiunganisha Familia ya Obama”

 

Vilevile Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Ida Odinga wametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Obama

Share with Others