Bodi ya korosho Nchini (CBT) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje imesema kuwa imepeleka taarifa za minada ya korosho kweye baadhi ya balozi inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Octoba mwaka huu 2020.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bodi ya korosho nchini (CBT) Francis Alfred alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Mkoani Mtwara.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba mpaka sasa Bodi hiyo tayari imepeleka taarifa za minada balozi 43 katika mataifa mengine kwa lengo la kutafuta wanunuzi wa zao hilo la Korosho.

Aidha Alfred ameongeza kuwa ni matumaini yao utaratibu huo utasaidia kuongeza idadi ya wanunuzi wa zao hilo la korosho licha ya kuwepo kwa janga la Virus vya Corona Duniani.

Mianada ya Korosho hapa nchini inatarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba mwaka huu 2020.

Share with Others