Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewaongoza viongozi mbalimbali, wakiwemo wabunge, mawaziri na wananchi, kumuaga aliyekuwa Rais hayati Dkt John Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka huu,Dar es alaam kutokana na tatizo la mfumo wa umeme kwenye moyo. 

Vilio na majonzi vimetawala katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, ambapo zoezi hilo la kutoa heshima za mwisho linaendelea kufanyika. 

Awali kabla ya zoezi la kuuga mwili wa Magufuli, kulitanguliwa na ibada ya misa takatifu .
 
Mkoa wa Dar es salaam utakamilisha zoezi la kuaga hapo kesho Machi 21, 2021, ambapo siku ya jumatatu viongozi wa nchi mbalimbali, wawakilishi wa jumuiya za kimataifa, mabalozi na wananchi wa mikoa ya kanda ya kati watashiriki zoezi la kuaga mwili, wakifatiwa na mikoa mingine na kisha kuzikwa siku ya ijumaa ya machi 26 nyumbani kwao chato Geita.

Share with Others