Wakulima wa zao la korosho Wilayani Liwale na Nachingwea mkoani Lindi chini ya chama kikuu cha Runali wamekubali kuuza korosho zao Kwenye mnada uliofanyika jana katika uwanja wa michezo wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.

 

Katika mnada huo jumla ya makampuni 28 yalijitokeza yakihitaji jumla ya tani 16,687 na kilo 65 ambapo chama cha Runali kilikuwa na jumla ya tani 1,998 na kilo 811.

 

Aidha katika mnada huo makampuni i 28 yaliyojitokeza yalinunua korosho kwa  bei ya juu ghala la Liwale Tsh 2,727 huku ya chini ikiwa 2677 ambapo kwa ghala la Nachingwea bei ya juu ilikuwa  2726 na ya chini 2700

 

Kwa upande wake Somoe Ngatumbula na Evast Malima wakizumza  kwa niaba ya wakulima wengine wamesema wamelidhika kuuza korosho zao  na wanatumaini uwepo wa bei mzuri kwa minada ijayo.

 

Nae mkuu wa wilaya ya Liwale,Sarah Chiwamba aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mnada huo amewataka wakulima hao kutumia pesa watazopata kwa kuwapeleka watoto shule, na kuandaa mashamba na kuwakumbusha kuwa makini hususani katika swala la utunzaji wa namba za siri ili kuepusha matapeli 

Share with Others