Mkuu wa wilaya Kilwa mkoani Lindi Christopher Ngubiagai ameziagiza AMCOS 11 wilayani humo, zilizopeleka korosho chafu zaidi ya tani 100 katika ghala kuu la Nangurukurru wilayani humo kwa Msimu wa mwaka 2019/2020 kwenda kuzichukua nakuziteketeza kutokana na Korosho hizo kukosa sifa ya soko la mazao ya biashara,na wale watakaoshindwa kuzichukua Korosho hizo watalazimika kuzilipia gharama za utunzwaji kwenye Ghala hilo.


Ngubiagai amezitaja AMCOS zinazotakiwa kwenda kufuata korosho hizo chafu kuwa ni pamoja na Kinjumbi, Pande, Somanga, Sisikwasisi, Ujirani mwema, Mikoma, Ulina, Matumbi,na Matandu,ambapo zimesababisha wakulima wengine kushindwa kulipwa fedha zao.


Sambamba na hilo mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa amesema katika msimu ujao wa ununuzi wa ufuta na korosho AMCOS yoyote itakayofanya uzembe katika kusimamia ununuzi itawachukuliwa hatua kali za kisheria kutokana na kuharibu soko.


Baadhi ya wakulima na viongozi wa kata ya Kinjumbi akiwemo diwani wa kata hiyo Ally Mawingu wamefurahishwa na tamko la mkuu wa wilaya hiyo, huku wakihamasishana kutoa taarifa za watu wanaoingiza mazao machafu katika vyama vyao vya msingi.

Share with Others