Watu watatu kutoka familia moja wilayani Ruangwa mkoani Lindi wameishi juu ya mti  tangu tarehe 24/1/2020 ambapo mvua kubwa ilianza kunyesha iliopelekea kufurika kwa maji kutokea mto mbwemkuru wilayani humo 

Mapema jana tarehe 28/1/2020 mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa aliambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa na kushiriki katika tukio la kuokoa watu walioishi katika miti kwa siku tano bila ya kupata chakula.

Akizungumza Mara baada ya kuwaokoa watu hao mkuu wa wilaya ya Ruangwa amewashukuru wananchi kwa kuendelea kujitoa katika kuwatafuta watu hao hadi kuwapata wakiwa juu ya miti,huku wakiwa hai.

Mkuu wa wilaya amesema huu ni mfano wa kuigwa na jamii kwa kuwa na umoja wakati wa matatizo.

Mwisho mkuu wa wilaya ya Ruangwa ameendelea kuwaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuendelea kuchukua tahadhari na waangalifu katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha

Share with Others