Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirroalipokuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020 amesema Magaidi zaidi ya 300 kutoka #Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji

Aidha ameongeza kwamba wamefuatilia na baadhi ya watu wamekamatwa huku wengine wakiwa raia wa hapa #Tanzania na wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo. Pia wengine waliofanya mauaji na kurudi Msumbiji nao wamekamatwa

Ameeleza kwamba, "Ukifanya uhalifu Tanzania na damu ya Mtanzania haiwezi kwenda hivi. Tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa"

IGP Sirro amesema watahakikisha wahalifu hao wanawakamata iwe wanakwenda Msumbiji, Kenya au kwingineko ili “mwisho wa siku haki itandendeka na kuwapeleka mahakamani.” 

Share with Others