Mfungale Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa Mwaka 1975 alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.1977  Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi na 1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India, baada ya hapo 1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam. kisha mwaka 1992 aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa, kisha  1994-1995 alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza.

Mwaka 2003 alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment ambapo baadae aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo akiwa masomoni Nchini Uingereza, mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini alianza kwa kutengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System.

2014 alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.

Mfungale ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja. 

Alibuni daraja la Magarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300. Hii ni orodha ya baadhi ya madaraja alioweza kujenga Patric Mfungale:

Daraja la Mkapa Rufiji
Daraja la Umoja linalounganisha tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
Daraja la Rusumo huko Mara
Daraja la Kikwete huko Magarasi.
Daraja la Nyerere huko Kigamboni
Mfugale kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.Pamoja na hayo amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258. Aidha kwa sasa mbali na kuwa mtendaji mkuu wa Tanroad Mfungale ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa pia ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.

Mwaka huu wa 2018 ametunzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Share with Others