Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameunda Kamati 3 zitakazobeba jukumu la kupambana na maambukizi ya Virusi vya #COVID-19 hapa nchiniKamati ya kwanza ambayo ni ya Kitaifa itahusisha Mawaziri mbalimbali wakiwemo Waziri ya Afya na Waziri wa Fedha (Bara na Zanzibar), Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Elimu, Waziri wa Mambo ya NjePia, Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Nchi Ofisi na Makamu wa Rais na wengine watakuwa katika Kamati hiyo ambayo itaongozwa na Waziri MkuuKamati ya pili itahusisha Makatibu Wakuu na itaongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi na itabeba jukumu la kufanya tathmini na kuishauri SerikaliKamati ya tatu ni Kikosi kazi cha Taifa na itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya. Wajumbe wa Kamati hii watakuwa washauri wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Share with Others