Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi  Christopher Ngubiagai amethibistisha kutokea kwa mlipuko wa gesi kituo cha Songasi wilayani humo na kusema kuwa “Hapa Kilwa Somanga kuna Power Station ambayo upande mmoja ni TANESCO na upande mmoja ni TPDC kwa maana Songas wana mtambo wao wa kupokea gesi kutoka Songosongo na Madimba inasafirishwa kwenda DSM, nimefika hapa nimekuta gesi imelipuka inaruka juu tukasimamisha magari yote yanayokwenda na yanayorudi, tumekubaliana njia zote 3 zifungwe”

 

Aidha Ngubiagai ameeleza kuwa 'na njia hizo ni  inayotoka Songosongo kuja hapa, njia ya bomba kutoka Madimba(Mtwara) na inayotoa gesi Muhoro kupeleka Kinyerezi zote zimefungwa na kwa kuwa ni usiku kuna kabaridi gesi imeanza kujichanganya na hewa na imepungua, baada ya saa moja tutaruhusu abiria kuendelea na safari, hakuna madhara kwa watu wala mali zao"

 

Mlipiko huo wa gesi umetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni na kusababisha baadhi ya barabara kufungwa huku umeme ukizimwa kuepuka athariyeyote inayoweza kujitokeza na watu  kuruhusiwa kuendelea na safari saa tatu baada ya tukio kutokea, pamoja na hayo hakuna majeruhi yeyote ambae ameripotiwa mpaka muda huu kutokana na mlipuko huo.

Share with Others