Imeelezwa kuwa kuzaa idadi ndogo ya watoto ni chanzo cha ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage ameyasema hayo leo wakati akielezea mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne.


Amesema aina hiyo ya saratani inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wagonjwa wengi huku waathirika wengi wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema wanawake wengi wa Dar es Salaam wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kutokana na kuzaa watoto wachache tofauti na ilivyo kwa wanawake wa mikoani.


“Ukizaa watoto wengi wakanyonya kuna uwezekano wa kupunguza hivyo vichocheo, huku mjini wanawake wako hatarini zaidi kwa sababu wanazaa watoto wachache,” amesema.


Dk Mwaiselage amezitaja sababu nyingine kuwa ni kutonyonyesha kwa muda unaostahili, matumizi ya pombe, unene uliopitiliza na kutofanya mazoezi.

Share with Others