Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka 2020 kuhusu furaha imewaorodhesha Wananchi wa Ukanda wa Afrika Mashariki kama baadhi ya watu wasiokuwa na furaha duniani.

Kenya iliorodheshwa nambari 121 kati ya 156 huku ikipata pointi 4.583 kwenye mizani ya pointi 10

Hata hivyo, ripoti hiyo iliyotolewa Ijumaa Machi 21, ilionyesha Kenya ndyo yenye watu walio na furaha zaidi ndani ya Afrika Mashariki.

Uganda walikuwa nambari 126, Burundi (140), Tanzania 148, Rwanda 150 na Sudan Kusini 152.

Ndani ya Afrika, Libya ndio nchi ambayo ina watu wenye furaha sana kwani ilikuwa nambari 80.

Wakenya wameorodheshwa nambari 121 kati ya mataifa 156 katika mizani ya furaha. Picha: John Ndichu

Ivory Coast nayo ilikuwa nambari 85, Benin 86, Congo 88, Ghana 91, Morocco 97 na Cameroon 98.

Afrika Kusini nayo ilishika nambari 109 ikiwa na pointi 4.814.

Kulingana na ripoti hiyo, Ufini ndiyo nchi yenye watu walio na furaha zaidi ulimwenguni ikifuatiwa na Denmark.

Wakenya hata hivyo wameorodheshwa kama watu wenye furaha sana Afrika Mashariki.

Marekani nayo iliorodheshwa nambari 18, Uingereza 13 Ujerumani 17, Italia nayo ikashikilia namabari 30.

Ripoti hiyo ilisema nchi zenye furaha zaidi zina hali nzuri ya mapato, uhuru wa wananchi, ukarimu, roho za kusaidiana kati ya mambo mengine.

Share with Others