Takwimu za Jeshi la Polisi katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019 zinaonesha kuwa magari binafsi ndiyo yamekuwa vinara wa kusababisha ajali zinazosababisha vifo na majeruhi wengi

Kwa mujibu wa Takwimu Rasmi, magari binafsi yamesababisha ajali 528, vifo 222 na majeruhi 453, kwa wastani; kila siku magari binafsi husababisha ajali tatu, kifo cha mtu 1 mpaka 2 na majeruhi 2

Kwa miezi sita ya mwanzo ya 2019 pikipiki zimesababisha ajali 334, vifo 176, majeruhi 319, kwa wastani pikipiki zinahusika katika ajali mbili kila siku na kusababisha kifo cha mtu mmoja mpaka wawili

Takwimu zingine zinaonesha mabasi ya abiria yalipata ajali 103, na kusababisha vifo 61 na majeruhi 195 katika kipindi hicho

Pia, ripoti hiyo inaonesha Malori yalihusika katika ajali 167, na kusababisha vifo vya watu 130 na majeruhi 142, wakati daladala zilipata ajali 143, na kusababisha vifo 89 na majeruhi 268

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, zaidi ya ajali 2,250 zimerekodiwa kuwa zilitokana na ulevi kati ya mwaka 2006 mpaka 2017 huku magari binafsi yakitajwa kuhusika zaidi kwenye ajali hizo

Share with Others