Maghala matatu ya chama cha ushirika UMOJA wilani Liwale mkoani Lindi yamebomoka na kusababisha korosho zilizokuwamo humo kumwagika kutokana na mrundikano wa uliopo katika maghala hayo.


Wakizungumza na Mashujaa Fm baadhi ya wakulima wa korosho wamesema kutokana na Korosho kuwa nyingi katika maghala hayo kumepekea kushindwa kuhimili mzigo uliopo na hatimae kubomoka. Pmoja na hayo wameiomba serikali kuitazama kwa umakini changamoto hiyo na kuona namna mzuri ya kuwasaidia wakulima ili wasipate hasara zaidi Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha umoja, HASSANI MPAKO amethibitisha kubomoka kwa maghala hayo matatu ya kukusanyia korosho na kueleza kuwa hatua hiyo ya kubomoka kwa maghala kumesababishwa na ukosefu wa magunia ya kuhifadhia Korosho. 


Aidha MPAKO ameongeza kuwa chama cha UMOJA kina tani 1600 ambazo zimekosa maguni hivyo amewashauri wakurugenzi wa halmashauri tatu zinazohudumiwa na RUNALI kutumia fedha za ushuru kwa ajili ya kununulia magunia ili kuweza kuokoa korosho za wakulima.

Share with Others