Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mkoa wa Lindi (lango) na taasisi zingine zikiwemo za kidini zimeombwa kujipanga na kuanza kuandaa jamii ya wakazi wa Lindi kuchangamkia fursa zinazokuja na mradi wa gesi asilia LNG utakaotekelezwa eneo la Likong’o manispaa ya Lindi.

Uandaaji huo ni pamoja na kuwaonyesha fursa na kuwaelekeza namna ya kuzitumia ili ziwanufaishe katika kubadilisha maisha yao.


Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi SHAIBU NDEMANGA wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya wadau mbalimbali muhimu wanaohusiana na mradi wa LNG, yaliyotolewa na Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mkoa wa Lindi (lango) kupitia mradi wao wa kuelekeza jamii namna ya unufaikaji wa pamoja wa rasilimali za umma juu ya sera ya unufaikaji na ushiriki wa wazawa (local content policy) katika masuala ya gesi na mafuta.

 

NDEMANGA amesema serikali ilitarajia kuona mabadiliko yanayoridhisha kutokana na fidi iliyolipwa kwa wakazi wa likongo’ wanaopisha mradi wa LNG ,lakini imekuwa tofauti kwani mabadiliko yaliyopo kwa wakazi wa maeneo yale amedai hayaendani na kiasi cha fedha walizolipwa,hivyo ni vyema wadau wa maendeleo wakawapa wakazi hao elimu ili wanufaike na fursa.

Share with Others