Redio Mashujaa fm leo imekabidhi viwekea taka (Dastbini) 7 vyenye thamani ya sh Mil 1,293,000 kwa Wilaya ya Lindi zitakazotumika katika kuimarisha usafi wa mazingira manispaa ya Lindi.


Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Lindi SHAIBU NDEMANGA ameipongeza Mashujaa Fm kwa
msaada huo na kuzikaribisha taasisi zingine kuiga mfano huo.

Awali meneja wa Mashujaa Fm Mkoa wa Lindi  ZAKIA WILIAM alisema moja ya maeneo ambayo wanatamani yangepewa kipaumbele kuwa ni Sokoni pamoja na  hospitali ya Rufaa ya Sokoine.
 

Mkurugenzi mtendaji katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Jomal Satura amesema kutokana na viwekea taka hivyo wataanzisha polisi jamii ambao watakuwa maalumu kwa kukamata watu wataokuwa wakitupa taka hovyo na kuwatoza elfu 50 kwa kila taka huku wakishirikia na Mgambo.

Hivi karibuni,Mashujaa Fm ilikabidhi fedha taslimu zaidi ya Mil 1,573,250 kwa shule ya msingi Kitomanga kwaajili ya kuchagiza ujenzi wa choo cha waalimu

Share with Others