Peju Jaiyeoba amesambaza vifaa laki tano vya kujifungua vilivyosalama nchini Nigeria -mfuko ulio na vifaa muhimu ili kuhakikisha kuwa wakina mama wanajifungua kwa njia salama na ilio safi.

 

"Mara nyengine mimi huwa nahisi kwamba siku moja kazi yetu haitahitajika tena", anasema Adepeju Jaiyeoba, mwanzilishi wa wakfu wa Brown Button nchini Nigeria."

 

Miaka saba iliyopita , Adepeju ama Peju kwa ufupi, ali acha kazi iliyokuwa ikimpatia kipato kizuri ya uwakili na kuanza kujifunza ukunga wa kitamaduni nchini Nigeria ili kuzalisha watoto.

Pia alitengeneza mfuko wa kuweka vifaa vya matibabu ambao umepata soko kubwa katika maeneo ya mashambani nchini Nigeria ukiokoa maelfu ya maisha.

Marafiki zake na familia walijaribu kumshauri asiache kazi yake ,lakini kifo cha rafikiye wa karibu wakati wa kujifungua hakikumpa chaguo mbadala.

''Rafiki yangu alikuwa ana elimu ya kutosha na ilinifanya mimi kuketi chini na kufikiria kwamba iwapo mtu ambaye ana uwezo wa kifedha anaweza kufariki wakati wa kujifungua, je ni nini kinachofanyika katika maeneo ya mashambani ambapo hawana vifaa vya kuzalisha?''

''Nilikuwa sina chaguo jengine kwani sikutaka kupoteza mtu mwengine tena. Sidhani kwamba hatua ya kujifungua mtoto inapaswa kusababisha kifo cha mtu mwengine''.

Share with Others