Imeelezwa kuwa Taifa linapoteza nguvu kazi yake ya baadae kutokana na wanafunzi wa kike kupata ujauzito wakiwa shuleni na kukatisha masomo yao sambamba na kukatisha malengo yao.

 

Hayo yamezungumzwa na mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu mkoa wa lindi juu ya changamoto za mimba za utotoni ambapo amesema mpaka kufikia sasa hali ya mimba za utotoni mkoani Lindi ni mbaya ambapo tayari mimba 151 zimeripotiwa 

 

Mapema leo walipokuwa wakizungumza na Mashujaa Fm kupitia kipindi cha Kuchele Mkuu wa wilaya ya Ruangwa na mkuu wa wilaya ya Nachingwea wameiomba jamii kujikita kwa nguvu katika kuhakikisha swala la mimba za utotoni linakoma,

 

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa amesema "Kuna kiwango standadi ambacho kinatakiwa cha kubeba ujauzito ukifatilia kwa taarifa huku kwetu tuna changamoto kubwa kwelikweli tuchukulie mfano kwa kesi ya mwaka jana kwa wilaya yangu ya Ruangwa ni Zaidi ya watu elfu moja ambao rika yao halipo katika utaratibu kwa kupata mimba"

 

Pamoja na hayo Mgandilwa amesema kwamba katika wilaya yake kwa kipindi cha mwaka 2018 mimba 17 ziliripotiwa wilayani Ruangwa ambapo kwa mwaka huu wa 2019 kuna idadi ya mimba 9 na  zote zimeripotiwa katika mamlaka husika 

 

Naye mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hashim Komba amesema kuwa wilayani Nachingwea kuanzia mwezi wa kwanza mpaka sasa ni matukio ya ubakaji 30 yameripotiwa huku mimba 21 zikiripotiwa ambapo sekondari ni mimba 15 na msingi ni mimba 6.

 

Kwa mujibu wa wataalam wa afya umri sahihi wa mwanamke kubeba mimba ni miaka 21 na kuendelea 

Share with Others