Mjadala wa kuibadilisha Katiba ya Kenya, lengo likiwa ni kubadilisha mfumo wa uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2022, umeanza tena.

Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na vinara wao Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanashinikiza, mabadiliko hayo kufanyika, huku wakitaka kuwe na Waziri Mkuu mwenye mamlaka na kuondoa wadhifa wa rais.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na William Ruto Naibu rais na wengine kutoka chama tawala wanaona hakuna haja ya hilo kufanyika.

Wakati huo huo, Naibu rais Ruto, amemshtumu kiongozi wa upinzani ambaye ni Raila Odinga kwa kutaka kumwondoa katika chama tawala cha Jubilee.

Share with Others