Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Gaspar Byakanwa amehalalisha upikaji na unywaji  wa gongo inayotengenezwa kwa mabibo kwani ni salama kwa matumizi ya binadamu. Amedai kuwa baada ya kupeleka sampuli za gongo ya mabibo kwa mkemia mkuu wa serikali majibu yamethibitisha kuwa haina madhara na inaweza kutumika kuzalisha spiriti iwapo itafikishwa viwandani 

 

Hata hivyo Byakanwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za Mtwara kuwasajili wapika gongo wote katika halmashauri zao ndani ya miezi miwili. Pia amewataka polisi kuacha mara moja kuwakamata wapikaji na wanywaji gongo.

 

Aidha Mkuu huyo wa mkoa wa Mtwara amemwandikia Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga kuanza kufanya mchakato wa maekebisho ya sheria ya pombe za kienyeji ili kuhalalisha gongo ya mabibo.

 

Pamoja na hayo amemwandikia Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa kutafuta wawekezaji ili waende Mtwara kujenga viwanda vya spirit na sanitizer kwa kutumia mabibo.

Share with Others