Mwanamuziki wa taarabu kutoka kundi la siti&the band anaeimba taarab asili na mziki wa kisasa maarufu kama Afro fussion amesema mara alipoanza kuimba mume wake pamoja na majirani walimbeza na kumkatisha tamaa kwa kile  anachokifanya.

Siti anasema hali hiyo imechangiwa na utamaduni wa kizanzibari,ambapo wengi walikua wanaamini mziki ni uhuni .

Pamoja na kupitia changamoto hizo Siti anadai hakukata tamaa katika sanaa ndipo alipoamua Kulea mwenyewe watoto wake kupitia kazi ya muziki.

Aidha,amesema changamoto hizo zimemfanya asimame na kuamini Kipaj chake jambo ambalo limempa mafanikio makubwa ,kushiriki katika matamasha mbalimbali likiwemo Sauti za busara ambalo limemsaidia kumkutanisha na wanamuziki kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Mwanamuziki huyo wa Siti & the band ambae hivi sasa anatamba na wimbo wake wa nielewe amesema kutokana na changamoto alizozipitia ametunga wimbo wa  nielewe ili kuelezea namna Wanawake wanavyopitia magumu katika maisha yao.

Share with Others