Mashujaa Group Ltd Kampuni inayomiliki Radio Mashujaa FM ya Lindi inatangaza nafasi za kazi: 
Kwa Watanzania wenye sifa stahiki katika maeneo yafuatayo:
1.    Chief Editor;   (Kituo cha kazi Lindi Mjini)
2.    Program Manager; (Kituo cha Kazi Lindi Mjini)
3.    Radio Producers; (Kituo cha kazi Lindi mjini)
4.    TV Producers; (Kituo cha kazi Mtwara Mjini)
5.    TV Presenters;    (Kituo cha kazi Mtwara mjini)    
Elimu/Taaluma na Uzoefu:
Certificate, Diploma na zaidi katika eneo husika;
Mhitimu katika fani yoyote aliye tayari kujifunza na kujiendeleza;
Wastaafu na wahitimu wapya wasio na uzoefu pia wanakaribishwa;
Wenye taaluma zaidi ya eneo moja watapewa kipaumbele.
Chief Editor ni LAZIMA awe na elimu isiyopungua Diploma ya Journalism/Mass Communication kutoka chuo kinachotambulika na TCU.
Wote hao wawe tayari kufanya kazi na kuishi Lindi na Mtwara.

Namna ya kuomba:
Wenye nia wanatakiwa kutuma maombi yenye barua, maelezo binafsi (CV) na 
nakala ya vyetu kwa barua pepe tu kwenda:-  jobs@mashujaafm.co.tz

**Tahadhari: Kughushi vyeti ni kosa la jinai na atakayethibitika kufanya udanganyifu wa aina hiyo atachukuliwa hatua za kisheria kabla au hata baada ya kupata ajira.

Share with Others