WAKAZI wa mtaa wa jangwani kata ya chikonji manispaa ya Lindi wamekumbwa na taharuki baada ya kitu kinachodaiwa kuwa ni ndege ya kishirikina kuanguka kwenye nyumba ya mkazi mmoja wa mtaa huo aitwae HAMZA CHIKAGO.


Tukio hilo limetokea Ijumaa Juni 5 2020 majira ya saa 8 usiku kufuatia ndugu zake wawili ambao pia ni waganga wa jadi waliotokea Newala Mkoa wa Mtwara kumtembelea na kuweka mitego iliyobaini kuwepo kwa matendo ya kishirikina katika mtaa huo.


Akizungumzia tukio hilo,CHIKAGO alisema ndugu zake hao walipofika nyumbani walianza kumweleza kuhusu mazingira ya kishirikina,ndipo alipochukua uamuzi wa kuwapeleka kwa mwenyekiti wa mtaa aliyemtaja kwa jina la IBRAHIMU SELEMANI kwa lengo la kuwatambulisha na kutoa tahadhari kuwa jambo lolote linaweza kutokea.


Ameongeza,ndugu zake hao wawili,walimweleza mwenyekiti wao ni waganga wa kutibu hivyo wanataka kuweka ulinzi katika nyumba ya ndugu yao na si kufanya shughuli za kiganga mtaani hapo licha ya baadhi ya watu kuanza kuwasumbua kwa kutumia nguvu walizodai ni za giza.

 

Kwa mujibu wa CHIKAGO mwenyekiti aliwaeleza,serikali haiamini mambo ya uchawi na kuhusu ulinzi wa nyumba,hilo ni suala binafsi ambalo kila mmoja anaweza kujiwekea kwenye nyumba yake.


Mashujaa fm ilipozungumza na mwenyekiti wa mtaa wa Jangwani IBRAHIMU SELEMANI ambaye alifika  eneo la tukio baada ya kupigiwa simu na baadhi ya watu,alipoulizwa endapo anafahamu kilichotokea,akashangazwa kwa kilichotokea kwakua hakutarajia watu hao kuibua taharuki kwa watu kwani alishazungumza nao kabla ya tukio hilo. 


Kwa upande wa wakazi wa mtaa huo wamedai kuelezwa na wataalamu wa jadi kuwa kitu hicho kina uwezo wa kubeba watu zaidi ya 360.

Share with Others