Kamati ya uchumi ya Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA), imesema karibu nusu ya watoto wote waliofariki chini ya miaka mitano walikuwepo barani Afrika.

Katibu mtendaji mkuu wa kamati ya ECA, Bi. Vera Songwe amesema hayo katika mkutano wa ngazi ya juu wa watunga sera, wasimamizi na wataalamu wa viwanda katika sekta ya dawa na biashara, uliofanyika katika makao makuu ya kamati hiyo huko Addis Ababa, Ethiopia.

Bibi Songwe ameeleza kuwa bara la Afrika haliwezi kujijengea na kuwa bara lenye ustawi kama kiwango cha juu cha vifo vya watoto namna hii.

Kwa mujibu wa takwimu za ECA, bara la Afrika lina asilimia 11 ya watu wote wa dunia, lakini linachangia asilimia 25 ya mzigo wa maradhi duniani

Share with Others