Upepo mkali unatokana Kimbunga Florence ambacho kinatishia watu wengi Marekani kimeanza kupigia maeneo ya pwani ya mashariki ya Marekani.
Maafisa wameonya kwamba huenda mawimbi makubwa ya kutoka baharini na mvua kubwa vikaathiri maeneo ya North na South Carolina, huku kimbunga hicho kikielekea maeneo ya bara.
Upepo wa kimbunga hicho unavuma kwa kasi ya maili 100 kwa saa (155 km/h).
Nyumba takriban 100,000 tayari hazina huduma ya umeme huku hali ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi pia 
watu zaidi ya milioni moja katika maeneo ya pwani North Carolina, South Carolina na Virginia walikuwa wametakiwa kuyahama makazi yao.
Maelfu walitafuta hifadhi katika vituo vya muda vya huduma za dharura Alhamisi usiku.
Watabiri wa hali ya hewa wametahadharisha kwamba maji ya mafuriko huenda yakafikia kina cha futi 13 (mita 4) na katika baadhi ya maeneo, huenda upepo mkali ukasababisha maji ya mito kuanza kurudi nyuma.
 

Share with Others