Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange ameonya nchi za kigeni kwa kile alichokitaja kuingiliwa katika masuala ya nchi yake, na kuomba kwa mara nyingine Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kuondoka nchini humo.
Kauli hiyo aliitoa katika mkutano Mkuu wa 73 wa Umoja w Mataifa huko New York nchini Marekani. Mkutano ambao ulianza tangu Jumanne wiki hii.
Joseph Kabila ameelezea ahadi yake kwa maadili yaliyotetewa na Umoja wa Mataifa, huku akishtumu baadhi ya nchi za kigeni kuingilia katika masuala ya ndani ya nchi yake.
Rais Kabila amesema DRC imekua sasa na amani na utulivu , huku akisisitiza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) kuanza kuondoa askari wake nchi humo.
‘Ni miaka ishirini baada ya kutumwa kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa katika nchi yangu na kwa sababu ya matokeo yao ambayo si mazuri katika mpango wa operesheni za kijeshi, Serikali yangu inaomba ikisisitiza vikosi hivyo vya Umoja aw Kimataifa kuanza kuondoka.”
Kauli hii inakuja wakati serikali ya DRC, hasa majeshi yake yakiendelea kukosolewa kushindwa kudhibiti usalama katika maeneo mengi ya nchi, hasa katika Mikoa ya Kivy Kaskazini, Kivu Kusini, na Tanganyika.
Baadhi ya askari wameshtumiwa kuhusika katika mauaji ya watu wasiokuwa na hatia katika maeneo mbalimbali, hasa katika mkoa wa Kasai na mji Kinshasa.

Share with Others