Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Joseph Pombe Magufuli ameibuka kidedea baada ya kujinyakulia tuzo ya ushindi katika kinyang’anyiro cha Ukombozi wa Afrika mara baada ya mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi Afrika kuonekana.
Ambapo katika Tuzo hiyo ya Ukombozi wa Afrika wamezingatia  kipengele cha elimu na Ujinga kama sehemu ya Ukombozi.

Na Tanzania imetolewa mfano kwa hatua iliyofikia ya kutoa elimu bure kutoka shule za msingi mpaka sekondari, na katika suala la umaskini kamati imeangalia hatua ya kuwajali watu wa kipato cha chini ambapo imeangazia hatua ya kuwasajili wafanyabiashara wadogo katika kuwatambua rasmi kwenye shughuli  zao na pia kuondolewa kodi za mazao kwa wananchi.

Share with Others