Juni 01 kila mwaka ni Siku ya Maziwa Duniani ambapo lengo kubwa huwa ni kuelimisha jamii kuhusu maziwa na umuhimu wake kama chakula ulimwenguni

Siku hii ilianzishwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) ili kutambua umuhimu wa maziwa na imekuwa ikisherehekewa kila Juni 01 tangu mwaka 2001

Kwa miaka michache iliyopita, India imetajwa kama mzalishaji mkubwa zaidi wa maziwa duniani ikizalisha zaidi ya tani Milioni 150. Maziwa na bidhaa za maziwa ni sehemu kubwa ya maisha nchini humo

Mwaka huu, kaulimbiu inasema "Miaka 20 ya Siku ya Maziwa", na kutokana na janga la CoronaVirus hakuna hafla kubwa zilizoandaliwa lakini washiriki wametakiwa kuzungumzia umuhimu wa maziwa pamoja na matatizo ya upatikanaji wake katika maeneo mbalimbali duniani

Hapa nchini, Naibu Waziri wa Kilimo na Ufugaji, Abdalah Ulega amesema kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mtu kwa mwaka ni wastani wa lita 47, kiwango ambacho ni kidogo kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO)

Naye Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Sophia Mlote amesema sekta ya maziwa Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kodi ambazo huongeza gharama za uzalishaji

Share with Others