makosa hayo ambayo yametajwa ni

1.  Uhaini
Hili ni kosa la jinai, Katika kifungu cha 39 (1) a,b,c,d,e, na F kimetaja kuwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mtu yeyote atakayejaribu kumuua rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kujenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri, kuhusu  kifo, kumlemaza, kumzuia, au kufungwa kwa rais, kumwondoa rais madarakani visivyo halali, kumwondolea rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali atakuwa  ametenda kosa la uhaini na ambaye atajenga, kusababisha au kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kupindua serikili iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama atakuwa ametenda kosa la uhaini na adhabu yake huwa ni kifo ikiwa itathibitika mahakamani
2 Ujambazi wa kutumia silaha
3 Mauaji
4 Kujihusisha na biashara za dawa za kulevya
5 Ugaidi
6. Usafirishaji wa fedha haramu
7. Mtuhumiwa aliyehukumiwa kifungo kinachozidi miaka mitatu
8. Aliyewahi kuruka dhamana

Share with Others