Rais Uhuru Kenyatta leo anaongoza Wakenya kusherehekea maadhimisho ya miaka 57 ya Sikukuu ya Madaraka (Madaraka Day), ambapo kwa mara ya kwanza yatafanyika kupitia mtandao

 

Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa CoronaVirus, wageni wachache wamealikwa kushiriki hafla itakayofanyika Ikulu jijini Nairobi na wananchi watafuatilia mtandaoni na vilevile kupitia matangazo ya moja kwa moja

 

Aidha, Raila Odinga ametoa pongezi kwa watumishi wa sekta ya afya kwa kuokoa maisha ya Wakenya. Pia amempongeza Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe kwa kuongoza vita dhidi ya COVID19

 

Kenya husherehekea sikukuu hii kila Juni 01, ikiwa ni kumbukumbu ya nchi hiyo kupata uhuru wa kujitawala

Share with Others