Watu takribani14 wameuwawa baada ya shambulio la wazi ndani ya kanisa nchini Burkina Faso, taarifa kutoka Serikalini zinasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo la jana ila idadi kamili haijatolewa

Waathirika wa shambulio hilo walikuwa wamehudhuria ibada katika kanisa la Hantoukoura, mashariki mwa nchi hiyo siku ya jumapili.

Idara ya usalama imekitaarifu chombo cha habari cha AFP kuwa watu wenye silaha ndiyo wamefanya shambulio hilo.


Chanzo kingine cha habari kimesema kuwa wanaume hao wenye silaha walitumia pikipiki na wameteketeza waumini, wachungaji na watoto waliokuwa kanisani.

Mwezi Oktoba, watu 15 waliuwawa na wawili walijeruhiwa vibaya katika shambulio lililotokea katika msikiti, hata hivyo mashambulio ya kigaidi yameongezeka nchini Burkina Faso tangu mwaka 2015.

Mamia ya watu wameuwawa katika taifa hilo katika miaka ya hivi karibuni zaidi na kundi la kigaidi la jihadist, kutokana na mvutano wa kikabila na kidini hasa katika mpaka wa Mali, eneo ambalo wanamgambo wa kiislamu walichukua eneo la kaskazini la nchi hiyo tangu mwaka 2012 kabla ya jeshi la Ufaransa kuwaondoa.

Share with Others