Tani 1,900,181 za wakulima wa korosho wa Mtama Lindi na Kilwa mkoani Lindi zinatarajiwa kuuzwa katika mnada wa Korosho endapo wakulima watakubaliana bei zitakazotajwa.

Mnada huo unafanyika katika chama cha msingi Chikonji na unatarajiwa kuanza majira ya saa 10.

Taarifa ya makusanyo ya Korosho na kiasi kilichoingizwa katika mnada huo iliyotolewa na meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao NURDIN SAID SWAHA imebainisha kuwa Korosho zitakazouzwa leo ni kutoka katika ghala za Nangurukuru ,Buco lindi ,na Ilulu Mtama.

Mapema mwanzoni mwa wiki hii,kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Lindi ROBERT NSUNZA ameiambia Mashujaa Fm kuwa ukusanyaji wa korosho za wakulima ulianza tangu tarehe 15 mwezi uliopita ingawa kuna changamoto ya vifungashio ambayo inaendelea kutafutiwa ufumbuzi.

Share with Others