Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imetangaza uchaguzi mdogo katika kata 37 za Tanzania bara zilizopo katika Halmashauri 27 nchini, ikieleza kuwa uchaguzi huo utafanyika Oktoba 13, 2018

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa fomu za uteuzi wa wagombea katika uchaguzi huo zitatolewa kati ya Septemba 15 hadi 21, 2018

Aidha, uteuzi wa wagombea utafanyika Septemba 21, 2018 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 12

Wakati huo huo, NEC imewateua madiwani watatu wa Viti Maalum kujaza nafasi zilizo wazi

Madiwani hao ni Halima Kisenga(CCM) katika Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni, Emmy Shemweta(CCM) katika halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Nuru Mwalimu Chuma(CUF) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
 

Share with Others