Serikali ya Uganda imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo ya Covid 19 kama mataifa mengine duniani ambapo mwaka jana Rais Yoweri Museveni alisema wanasayansi wa Uganda wanajaribu kufanya utafiti kuanza kutengeneza chanjo yao na tiba ya Covid-19 ambayo tayari iko kwenye majaribio.

''Ninafanya kazi na watu wangu kuanza kutowa chanjo yetu, sio kwamba tumekaa tu kusubiri watusaidie, tumechelewa lakini sasa tumeanza na chanjo yetu itakwenda kote duniani'' Rais Museveni.

Ameeendelea kusema: ''Tutaanza kufanyia majaribio panya mwezi wa june kuona kama ina madhara na baadae mwezi wa Augosti tutafanyia majaribio nyani na kusubiri kudhibitishwa na WHO.''

Rais Museveni ametowa kauli hiyo wakati alipodungwa sindano ya chanjo ya Covid-19 ya #AstraZeneca pamoja na na mkewe Janet Museveni, katika ikulu ya rais Nakasero mjini Kampala.

Aidha Rais huyo ametowa wito kwa wananachi kujitokeza kupata chanjo kwani haina madhara

Share with Others