Viongozi wa mataifa ya Ethiopia na Eritrea wameshuhudia kufunguliwa kwa mpaka huo muhimu ambao ulikuwa umefungwa kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita kufuatia mzozo wa mpakani.
Hatua hiyo ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, hali ambayo itaiwezesha Ethiopia kutumia bandari ya Assab.
Kituo kingine cha mpakani kilichopo karibu na mji wa Zalambessa nchini Ethiopia pia kinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Mkataba wa amani uliyotiwa saini na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mwezi Julai  ndio umechangia kufufua uhausiano wa kidiplomasia na wa kibiashara.
Kufunguliwa kwa mpaka huo kunajiri wakati Ethiopia inasherehekea mwaka mpya.
 

Share with Others