Vita vya maneno kati ya Naibu wa rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga vimeibuka tena huku matamshi ya Ruto kumhusu Raila Odinga yakizua hisia kali miongoni mwa viongozi wanaomuunga mkono Raila.

Hii ni kufuatia matamshi ya Ruto kwamba Raila anayumbisha chama cha Jubilee.


Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema matamshi ya Naibu rais William Ruto, anamfanyia njama ya kumfukuza ndani ya chama tawala cha Jubilee, ni hofu aliyonayo kuhusu vita dhidi ya ufisadi. Odinga amesema ushirikiano wake na rais Uhuru Kenyatta kuhimiza umoja wa kitaifa na kupambana na ufisadi hautarudi nyuma.


Wakati huo huo wanasiasa wa ODM wamemshtumu William Ruto kuwa hana heshima kwa Raila Odinga huku 
Wadadisi wa siasa nchini humo wakiona kuwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2022, huenda hatima ya uongozi wa Nchi utaamuliwa na wanasiasa hao wawili.
 

Share with Others