Waajiri nchini Tanzania wametakiwa kutenga muda wa kuwasikiliza wafanyakazi wao ili kuondoa majungu maofisini


Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama wakati akizungumza na baraza kuu la wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma leo 


Mhagama ambaye ni mbunge wa jimbo la Peramiho  amesema bila kuwapa nafasi watumishi kwa kuwasikiliza, itawapa nafasi kuzungumzia nje ya ofisi jambo linaloweza kuwa hatari kwa taasisi.


"Maridhiano na majadiliano katika taasisi yoyote ni jambo la msingi sana, lazima mtoe nafasi kwa watu ili wapumue maana mkiwaacha na nyongo itakuwa jambo baya sana katika ustawi wa taasisi na mtakosa maelewano," amesema Mhagama.


Amewataka wafanyakazi kuwajibika ipasavyo kabla ya kudai haki zao kwani haki bila wajibu haitawezekana na si jambo jema.
Waziri huyo amekumbusha wasichana kusoma hesabu ili kuongeza idadi ya watumishi wanawake katika ofisi za takwimu.
 

Share with Others