Baadhi ya Wafanyabiashara Soko Kuu Mkoani Mtwara wamelazimika kufunga vibanda vyao vya Biashara kwa ukosefu wa wateja hali iliyopelekea kuishiwa mitaji yao,

Mpaka sasa Zaidi ya vibanda 20 vimefungwa kwa kukosa mitaji  hiyo huku sababu kubwa ikitajwa kupungua kwa wateja sokoni hapo.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo wameshauri juu ya kupunguzwa kwa kodi zinazowakabili  ili iweze kuendana na kipatao chao ambapo mpaka sasa wanalazimika kutoa kodi ya Halmashauri ,TRA , Pamoja na Kodi ya wasimaminzi wa soko hilo  (WABISOKO).

Awali wafanyabaishara hao walisema kuwa kwa sasa biashara yao imezidi kuwa ngumu baada ya kuongezeka wafanyabiashara wengine sokoni hapo pamoja na ongezeko la pango ya vibanda  ambapo kwa mwezi wanalizimika kulipia laki moja na nusu mpaka laki mbili huku kipato kinachopatikana kikiwa hakilingani na matumizi yao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa soko Ramadhani Hassani alisema kuwa sababu ya kufungwa vibanda kwa kiasi kikubwa imechangiwa na mzunguko mdogo wa biashara Mkoani Mtwara

Share with Others