Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema, Serikali haijaacha kuwalipa watumishi wake katika kipindi hiki cha #CoronaVirus kwasababu iko vizuri kiuchumi na kuongeza kuwa hilo linalotakana na sababu kwamba nchi jirani na Tanzania zimepunguza mishahara ila Tanzania wafanyakazi wanapata mishahara yao bila kuchelewesha 

Aidha amebainisha kwamba pamoja na corona kugusa kwa asilimia kubwa uchumi na sekta nyingine hatua zilizochukuliwa zimeiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuulinda uchumi wa nchi.

Dkt. Abbas ameongeza kuwa kuusu hali ya maambukizi ya #CoronaVirus kwa nchini yamepungua sana, Watu wengi wanapima na amebainisha kuwa takwimu zinaonesha Wagonjwa hawafiki 60 kwa Tanzania

Aidha ameongeza kuwa vipimo vya sasa vikitoa majibu vinaaminika zaidi kuliko vile vya awali ambavyo vilitoa majibu ya Mapapai na Mbuzi wakiwa wameathirika na virusi hivyo

Amemalizia kwa kusema , “Nchi nyingi zimebadili mkakati wa utoaji taarifa, nyingi zimeacha kutoa taarifa za COVID19. Tumebadili sababu tunaamini Watanzania wameelewa lakini pale kwenye umuhimu tutaendelea kukumbushana”

Share with Others