Wanafunzi watano katika kaunti za #Nakuru, Samburu na Nyandarua Nchini Kenya wamelazimika kufanyia mitihani yao ya Darasa la Nane (KCPE), Hospitalini baada ya kujifungua Watoto hapo jana (Jumatatu)Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Nakuru, Bw Fredrick Osewe amesema mmoja wa watahiniwa hao mwenye umri wa miaka 15 kutoka Shule ya Msingi ya Kuresoi, iliyopo Kaunti Ndogo ya Kuresoi Kaskazini, alikimbizwa Hospitalini baada ya kuanza kulalamikia maumivu wakati akiwa Shuleni Hata hivyo imetajwa kuwa katika Kaunti ya Nyandarua, Watahiniwa 18 walipata mimba wakati Wanafunzi wakiwa majumbani kutokana na janga la virusi vya Corona mwaka 2020 hivyo Watahiniwa 11 wanafanya mtihani huo wakiwa Wajawazito

 


Aidha, Katika kaunti hiyo hiyo, mtahiniwa (17) kutoka eneo la Njoro anafanyia mtihani wake akiwa mikononi mwa Polisi kwa tuhuma za kumdhalilisha kimapenzi  mtoto wa miaka 11 katika kijiji cha Sigotik eneo la Nessuit kaunti ndogo ya Njoro ambapo Mshukiwa huyo baada ya kufikishwa mahakani  aliachiliwa kwa dhamana ya Sh400,000 na mdhamini wa kiasi kama hicho au bondi Sh300,000 pesa taslimu.

 

 

Share with Others