Wafanyabiashara na wananchi kutoka soko la Feri Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara wameruhusiwa kuendelea na ujenzi wa msikiti unaojengwa katika eneo hilo.

 

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwra Dunstan Kyobya alipotembelea na kufanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo.

 

Awali Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani Emmanuel Mwaigobeko alisimamisha ujenzi wa msikiti huo kutokana na wananchi wa eneo hilo kukiuka makubaliano ya awali ambapo walikubaliana kujengwa kwa msikiti wa muda.

 

Licha ya kutolewa kwa agizo hilo la kuendelea kwa ujenzi wa msiti huo Mkuu huyo wa Wilaya amewasihii wafanyabiashara na wananchi wa eneo hilo muda wowote Serikali watakapolihitaji eneo hilo wawe tayari kulikabidhi.

 

Huu ni mwendelezo wa Mkuu huyo wa Wilaya wa Mtwara Dunstan Kyobya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya wilaya yake kusikiliza na kutatua kero zao katika maeneo wanayoishi.

Share with Others