Wiki chache baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Malawi, Rais  Lazarus Chakwera amepata upinzani mkubwa baada ya ya raia wa Taifa hilo kuanza maandamano dhidi yake wakimkosoa kuteua watu ambao ni ndugu kwenye Baraza la Mawaziri


Rais Chakwera anadaiwa kuteua baadhi ya Mawaziri akiwemo mume na mke na wengine ni kaka na dadaake huku 70% ya Baraza hilo ikidaiwa kuhusisha watu wa jamii moja na yeye


Mwanaharakati wa masuala ya kijamii, Mkotama Katenge Kaunda alisema hatua hiyo inakera kwa kuwa Rais aliahidi kwamba Malawi mpya itakabiliana na upendeleo na ukiritimba

 

Rais huyo mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Rais Mutharika kwa asilimia 58.57 ya kura katika Uchaguzi wa marudio

Share with Others