Mahakama ya Lyon nchini Ufaransa imewakuta na hatia raia wawili kutoka nchi hiyo wenye umri zaidi ya miaka hamsini kwa kupanga mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Congo-Brazzaville.
Wawili hao, waliozaliwa mwaka 1961 na 1967, wameshtakiwa kwa kosa la "kushirikiana na kundi la wahalifu" na "kumiliki vilipuzi" na wamewekwa chini ya udhibiti wa mahakama. lakini ofisi ya mashitaka imesema haikubaliani na uamuzi huo wa mahakama na imekata rufaa, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama.
Mtu wa tatu, aliyezaliwa mwaka 1962, aliwekwa kama shahidi atakayesaidia kutoa mwanga mbele ya mahakama.
Mahakama inawashtumu kuwa walipanga kumuua "katika wiki zijazo" mwanasiasa wa upinzani wa Congo-Brazzaville, anayeishi katika mkoa wa Paris. Mwanasiasa huyo hakutajwa na mahakama, hata majina ya washtumiwa wa mauaji hayo hayakutajwa.
 

Share with Others